Friday, January 21, 2011

ZAWADI YA BITHDAY KUICHELEWESHA SENIOR BACHELOR

 Mwaka 2011 kiukweli umeanza kwa kasi ya ajabu katika tasnia ya film Tanzania kwa kuwa kila mmoja amepanga kufanya vizuri kwa upande wake. Maneno hayo yalisemwa na msanii maarufu na mwenye uwezo wa hali ya juu Jackob Steven(JB). Jb ambaye aliwahi kutangaza kuwa filamu yake ya SENIOR BACHELOR itatoka mwezi wa 2 mwaka huu, sasa ameibuka tena na kusema filamu hiyo itachelewa kidogo kutoka mpaka mwezi wa 4 mwaka huu.Kiukweli nilipanga kuitoa mwezi wa 2 kwani kwa sasa iko katika hatua ya mwisho ya subtitle ambayo hadi kufikia mwisho wa mwezi huu itakuwa tayari. (alisema jb). Kulingana na soko letu la Tanzania inabidi itoke mwezi wa 4 kwa sababu tayari kuna filamu yangu nyengine sokoni inayoitwa ZAWADI YA BIRTHDAY ambayo ilitakiwa kutoka mwezi huu lakini kutokana na sababu zilizo nnje ya uwezo wangu inabidi filamu hiyo itoke mwezi wa 2. (aliongeza). Lakini ninachowaambia mashabiki wangu na wapenzi wa filamu bongo wakae mkao wa kula kwani filamu hiyo ya ZAWADI YA BITHDAY nayo ni kali zaidi ya moto wa gesi kwani imechezwa na wasanii wenye uwezo wa hali juu. Hebu vuta picha tukutane pamoja mimi, Richie, Adam Kuambiana na Shamsa Ford  huo moto unadhani utakuwaje? So watu wakae tayari kuipokea kwani ni kali vibaya.
 JB akipika chapati kwenye moja ya scene katika filmu ya SENIOR BACHELOR.
 Huu sio ugomvi jamani, hawa ni wasanii Jack Pentzel na Sudy wakiwa kwenye scene katika filamu ya SENIOR BACHELOR.
 Director wa SENIOR BACHELOR Single Mtambalike(RICHIE) na  production manager Suleiman Said Barafu wakijadili kitu.
Jb akisubiri maelekezo kutoka kwa director ili aanze makamuzi. kwa kweli filamu hii ina matukio mengi tofauti tofauti.

No comments:

Post a Comment