Ili kurudisha heshima yangu kwa wadau na mashabiki wangu katika tasnia hii ya filamu ni lazima nifanye mambo ambayo ni hakika yatarudisha heshima kwangu. Maneno hayo yalisemwa na Single Mtambalike mkurugenz wa BULLS ENTERTAINMENT, pia ni muigizaji aliyewahi kupata tuzo ya muigizaji bora wa kiume miaka kadhaa iliyopita. Kwa hakika mwaka huu ndo mwaka wa kurudisha heshima kwani baada ya filimu ya SKENDO itakapotoka mwezi february mwaka huu, mashabiki wangu watapata kuniona kwa mara ya kwanza nikitoka na watoto wangu wawili Prince Mtambalike na Darlene Mtambalike ambao kwa muda mrefu nimekuwa nikiwapika kisanaa na sasa ndo muda wao wa kutoka. Filamu hiyo itakayokwenda kwa jina la USWAHILINI itakuwa ni moto wa kutea mbali kwani watu waliocheza humo wote wamecheza kwa kiwango cha juu sana.Baada ya SKENDO kutoka nitawatangazia mashabiki kuwa filamu hii itatoka lini.
Darlene Single Mtambalike katika pozi
Prince Single Mtambalike katika pozi
No comments:
Post a Comment