Friday, February 4, 2011

BAADA MUDA MREFU SASA 5EFECT MOVIES KUFANYA KAZI NA RICHIE

 Kwa kweli amini usiamini lakini ukweli ni kwamba tangu ianze tasnia ya filamu hapa Tanzania haikuwahi kutokea kampuni ya 5efect movies kufanya kazi na RICHIE. Mkurugenzi wa 5efect movies bw Wiliam j Mtitu safari hii ameamua kufanya kazi na Richie. Nimeamua kufanya kazi na Richie kwa sababu ni msanii mzuri na mwenye kiwango cha hali ya juu.(Alisema Mtitu)
 Richie akiwa katika scene
 Camera man Denic, Richie na msanii chipukizi lizzy wakiwa mzigoni.
 Richie na Lizzy kwenye scene.
 Single Mtambalike au Richie, pi wasanii wenzie wanamuita DENZEL wa bongo hapa akikamua
Kwa kuwa Richie ni director wakati mwengine aliingilia kati kuelekeza. hapa alikuwa akimuelekeza lizzy jinsi ya kucheza.

Friday, January 21, 2011

ZAWADI YA BITHDAY KUICHELEWESHA SENIOR BACHELOR

 Mwaka 2011 kiukweli umeanza kwa kasi ya ajabu katika tasnia ya film Tanzania kwa kuwa kila mmoja amepanga kufanya vizuri kwa upande wake. Maneno hayo yalisemwa na msanii maarufu na mwenye uwezo wa hali ya juu Jackob Steven(JB). Jb ambaye aliwahi kutangaza kuwa filamu yake ya SENIOR BACHELOR itatoka mwezi wa 2 mwaka huu, sasa ameibuka tena na kusema filamu hiyo itachelewa kidogo kutoka mpaka mwezi wa 4 mwaka huu.Kiukweli nilipanga kuitoa mwezi wa 2 kwani kwa sasa iko katika hatua ya mwisho ya subtitle ambayo hadi kufikia mwisho wa mwezi huu itakuwa tayari. (alisema jb). Kulingana na soko letu la Tanzania inabidi itoke mwezi wa 4 kwa sababu tayari kuna filamu yangu nyengine sokoni inayoitwa ZAWADI YA BIRTHDAY ambayo ilitakiwa kutoka mwezi huu lakini kutokana na sababu zilizo nnje ya uwezo wangu inabidi filamu hiyo itoke mwezi wa 2. (aliongeza). Lakini ninachowaambia mashabiki wangu na wapenzi wa filamu bongo wakae mkao wa kula kwani filamu hiyo ya ZAWADI YA BITHDAY nayo ni kali zaidi ya moto wa gesi kwani imechezwa na wasanii wenye uwezo wa hali juu. Hebu vuta picha tukutane pamoja mimi, Richie, Adam Kuambiana na Shamsa Ford  huo moto unadhani utakuwaje? So watu wakae tayari kuipokea kwani ni kali vibaya.
 JB akipika chapati kwenye moja ya scene katika filmu ya SENIOR BACHELOR.
 Huu sio ugomvi jamani, hawa ni wasanii Jack Pentzel na Sudy wakiwa kwenye scene katika filamu ya SENIOR BACHELOR.
 Director wa SENIOR BACHELOR Single Mtambalike(RICHIE) na  production manager Suleiman Said Barafu wakijadili kitu.
Jb akisubiri maelekezo kutoka kwa director ili aanze makamuzi. kwa kweli filamu hii ina matukio mengi tofauti tofauti.

Tuesday, January 11, 2011

USWAHILINI KUJA BAADA YA SKENDO

 Ili kurudisha heshima yangu kwa wadau na mashabiki wangu katika tasnia hii ya filamu ni lazima nifanye mambo ambayo ni hakika yatarudisha heshima kwangu. Maneno hayo yalisemwa na Single Mtambalike mkurugenz wa BULLS ENTERTAINMENT, pia ni muigizaji aliyewahi kupata tuzo ya muigizaji bora wa kiume miaka kadhaa iliyopita. Kwa hakika mwaka huu ndo mwaka wa kurudisha heshima kwani baada ya filimu ya SKENDO itakapotoka mwezi february mwaka huu, mashabiki wangu watapata kuniona kwa mara ya kwanza nikitoka na watoto wangu wawili Prince Mtambalike na Darlene Mtambalike ambao kwa muda mrefu nimekuwa nikiwapika kisanaa na sasa ndo muda wao wa kutoka. Filamu hiyo itakayokwenda kwa jina la USWAHILINI itakuwa ni moto wa kutea mbali kwani watu waliocheza humo wote wamecheza kwa kiwango cha juu sana.Baada ya SKENDO kutoka nitawatangazia mashabiki kuwa filamu hii itatoka lini.
 Darlene Single Mtambalike katika pozi
Prince Single Mtambalike katika pozi

Monday, January 3, 2011

SKENDO PROMO





 Skendo ni filamu inayotarajiwa kuingia sokoni mwezi wa 3 mwaka huu. Niliwahi kuzungumza katika blog hii kuwa itakuwa ni kali na yenye mabadiliko makubwa sana ukilinganisha na filamu nyingi zilizowahi kuonekana mwaka uliopita. Ili kuthibitisha hilo hebu angalia hii treiler kisha unipe maoni yako kupitia blog hii.